Serikali yaombwa kuwachukulia hatua kali wanaofanya vitendo vya ukatili
9 August 2023, 5:32 pm
Picha ni Mkazi wa jiji la Dodoma akizungumzia sheria zinazopaswa kuchukuliwa kwa watu wanaofanya vitendo vya ukatili. Picha na Aisha Shaban.
Takwimu zilizotolewa na Jeshi la Polisi zinaonyesha kuwa kuanzia Januari hadi Juni 2021 watu 15131 walifanyiwa ukatili wa kijinsia huku ripoti hiyo ikionyesha ongezeko la mauaji kwa wanawake walio katika ndoa.
Na Aisha Shaban.
Serikali imeombwa kuchukua hatua kali za kisheria kwa watuhumiwa wote wa vitendo vya ukatili ili kupunguza kukithiri kwa matukio hayo ndani ya jamii.
Kufuatia vitendo hivi kuendelea kuripotiwa mara kwa mara katika maeneo mbalimbali nchini Dodoma tv imefanya mahojiano na baadhi ya wananchi wa Jijiji la Dodoma na nimeanza kwa kuwauliza je nini kifanyike ili kutokomeza vitendo hivi?
Hapa Bw. David Sayoni ni mmoja wa viongozi katika soko kuu la majengo jijini Dodoma anatueleza juu ya aina ya ukatili wanaokumbana nao katika maeneo ya biashara.
Dodoma Tv imemtafuta Sheikh kutoka msikiti wa Majengo Adam Sadik ambae anatumia fursa hii kukemea vitendo vya ukatili katika jamii kwani ni kinyume na mafundisho ya dini.
Ripoti iliyotolewa Septemba 2021 na Jarida la Afrika kuhusu hali ya ukatili wa kijinsia Tanzania miongoni mwa wanandoa, imeonyesha kuwa, asilimia 46 ya wanandoa hufanyiwa ukatili wa kijinsia, ambapo asilimia 36 walifanyiwa ukatili wa kimwili na asilimia 32 walifanyiwa ukatili wa kisaikolojia na asilimia 13 walifanyiwa ukatili wa kingono.