Kongamano la maendeleo ya vijana kuanza Agosti 3
2 August 2023, 4:27 pm
Kongamano hilo linatarajiwa kufanyika kwa siku mbili tarehe 3 na 4 ya mwezi Agosti likiwa na lengo la kuwakutanisha vijana kutoka maeneo mbalimbali nchini .
Na Fred Cheti.
Serikali kupitia Wizara ya Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) kwa kushirikiana na taasisi mbalimbali za vijana imeandaa kongamano la maendeleo kwa vijana.
Kongamano hilo linatarajiwa kufanyika kwa siku mbili tarehe 3 na 4 ya mwezi wa nane likiwa na lengo la kuwakutanisha vijana kutoka maeneo mbalimbali nchini kwa lengo la kujadili mambo mbalimbali yanayowahusu katika nyanja zote za kijamii na kiuchumi kama ambavyo anaeleza mwenyekiti wa kongamano hilo Bwana Rajabu Nunga ambaye ni Mkurugenzi wa DOYODO.
Kwa upande wake mwakilishi kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Ajira na wenye Ulemavu ambaye ni Afisa Vijana Mwanadamizi Amina Sanga amesema kuwa kongamano hilo ni utekelezaji wa sera ya vijana.
Naye Mkurugenzi wa shirika la Freedom House Tanzania Bwana Daniel Lema ambaye ni mratibu wa kongamano hilo anaelezea mambo mabalimbali zikiwemo mada zitakazojadiliwa katika kongamano hilo.