Bodi mpya yatakiwa kusimamia kanuni, taratibu
28 July 2023, 2:41 pm
Pia amesema wana jukumu la kuishauri wizara kujua ni namna gani Wakala wa Vipimo iboreshe utendaji kazi wake.
Na Seleman Kodima.
Waziri wa Viwanda na Bashara Mhe. Dkt Ashatu Kijaji amewataka wajumbe wapya wa bodi ya sita ya ushauri ya Wakala wa Vipimo nchini kusimamia sheria, kanuni na taratibu katika utekelezaji wa majukumu yao mapya.
Waziri Kijaji ametoa agizo hilo wakati akizindua bodi ya sita ya ushauri Wakala wa Vipimo katika hafla iliyofanyiwa ukumbi wa Mkandarasi jijini Dodoma.
Dkt Kijaji ameitaka bodi hiyo kufanya kazi kwa weledi na iwapo watakwama basi watoe taarifa mapema.
Aidha Dkt Kijaji ameitaka bodi hiyo kuhakikisha watanzania wanaifahamu vyema wakala wa vipimo kupitia bidhaa ambazo zina vipimo sahihi .
Akitoa neno la shukrani, mwenyekiti wa bodi ya sita ya ushauri ya wakala wa Vipimo ambaye ni Afisa Mtendaji wa mkuu wa Wakala wa Vipimo Bi Stella Kahwa amemuhakikishia waziri kuwa kupitia ushirikiano wao na menejimenti watahakikisha wanazitatua changamoto zote zinazolalamikiwa na wananchi