Ukosefu wa zahanati Mbelezungu Chamwino wapelekea vifo vya akina mama wajawazito
11 July 2023, 6:08 pm
Sera ya afya ya mwaka 2007 imeweka wazi kuwa kila kijiji kanatakiwa kuwa na zahanati moja ili kuhudumia wananchi wa eneo hilo.
Na Victor Chigwada.
Imeelezwa kuwa ukosefu wa Zahanati katika kijiji cha Mbelezungu Wilayani Chamwino ni sababu inayosababisha vifo vya akina mama wajawazito .
Hayo yamebainika baada ya kituo hiki kuzungumza na wakazi wa eneo hilo ambapo wamesema kukosekana kwa zahanati katika kijiji hicho kunachangia baadhi ya akina mama wajawazito kupoteza maisha kutokana na umbali wa upatikanaji wa huduma ya mama na mtoto .
Akizungumzia Changamoto hiyo Diwani wa Kata hiyo Bw.Musa Omary amekiri uwepo wa Zahanati mbili katika Kata hiyo hali ambayo bado ni changamoto kwa wananchi wanaokaa mbali na maeneo yanayopatikana zahanati hizo
Kwa upande mwingine Diwani Huyo amesema kuwa licha ya uwepo wa zahanati hizo mbili lakini wanaupungufu wa wahuduma wa afya hali inayosababisha msongamano wagonjwa kwa nyakati tofauti