STAMICO kuanza kuzalisha nishati mbadala
10 July 2023, 5:32 pm
Mkurugenzi Mtendaji wa shirika hilo Bwana Venance Mwase akizungumza na vyombo vya habari .Picha na Fred Cheti.
Matumizi ya mkaa na kuni yanatajwa kuchangia uchafuzi na uharibifu wa mazingira.
Na Fred Cheti.
Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) linatarajia kuanza kuzalisha nishati ya mkaa mbadala kwa ajili ya kupikia ambao unaelezwa kuwa rafiki kwa mazingira.
Hayo yameelezwa na Mkurugenzi Mtendaji wa shirika hilo Bwana Venance Mwase ambapo amesema mkaa ni rafiki kwa mazingira na unazalishwa kwa ubora wa hali ya juu bila ya kuwa na athari za kiafya kwa mtumiaji.
Mkugenzi huyo ametoa rai kwa watanzania kuachana na matumizi ya kuni na mkaa ambayo yanatajwa kama uchafuzi wa mazingira na kuanza kutumia nishati mbalimbali mbadala zinazozalishwa.