REA yafikisha umeme vijiji vyote 87 Kongwa
3 July 2023, 5:37 pm
Mradi wa kusambaza umeme katika Maeneo ya pembezoni mwa miji awamu ya pili wilayani kongwa umegharimu Bilion Moja Milion miatano themanini na tatu laki nane tisini na tisa elfu mia nne sabini na nane na senti sita 1,583,899,478.06
Na Mindi Joseph.
Jumla ya Vijiji 87 na Vitongoji 268 Wilayani kongwa vimefikiwa na huduma ya umeme kupitia wakala wa nishati Vijijini REA.
Wilaya ya kongwa ina jumla ya vitongoji 383 na katika ujenzi wa mtandao wa umeme vitongoji 115 vilivyobaki bado unaendelea na vitongoji 15 vipo katika mpango wa kupatiwa umeme kwa mwaka wa fedha 2023/2024.
Mhandisi Nasma Ibrahim Kivina ni msimamizi wa Mradi wa REA Mkoani Dodoma ameyabainisha hayo katika Hafla ya Uwashwaji wa umeme katika Kitongoji cha Chang’ombe Kijiji cha Laikala Wilayani kongwa.
Kwa upande wake Mbunge wa jimbo la Kongwa, Job Ndugai amepongeza kazi kubwa inayofanywa na wakala wa Nishati Vijijini REA huku akiwahimiza wananchi kuvuta huduma ya umeme kwa kila kaya.
Nao baadhi ya wananchi walikuwa na haya ya kusema baada ya umeme kuwashwa katika kitongoji chao.