Halmashauri ya jiji Dodoma kugawa viwanja 1,035 kama fidia
3 July 2023, 2:15 pm
Mwaka wa fedha ujao 2023/2024 halmashauri inatarajia kupima takribani viwanja 6,000.
Na Fred Cheti.
Halmashauri ya jiji la Dodoma inatarajia kugawa jumla ya viwanja 1,035 kwa kufidia na kuwapunguzia wananchi wanaodai viwanja takribani viwanja 3,995 eneo la Nala.
Hayo yameelezwa na mkurugenzi wa jiji la Dodoma Bwana John Kayombo wakati akizungumza na baadhi ya wananchi wenye changamoto za viwanja pamoja na baadhi ya watendaji wa ardhi wa jiji pamoja na Waziri wa Ardhi Mh Angelina Mabula ambapo amesema Kamati ya Ugawaji Ardhi imeshakaa na tayari wamekubaliana kugawa viwanja hivyo.
Aidha mkurugenzi huyo amesema kuwa kwa mwaka wa fedha ujao 2023/2024 halmashauri inatarajia kupima takribani viwanja 6,000 huku viwanja 2,960 vikitarajiwa kugawiwa wananchi kwa ajili ya kukamilisha changamoto ya viwanja ambavyo wananchi wanavidai.