AMDT yawakutanisha wabunge wa Lindi, Mtwara kujadili zao la alizeti
27 June 2023, 7:37 pm
Taasisi ya kuboresha Mifumo ya Masoko ya Kilimo Tanzania katika kuinua sekta ya kilimo nchini, imeamua kuanza na mikoa ya Lindi na Mtwara kulifanya zao la alizeti kuwa zao la kimkakati katika mikoa hiyo.
Na Mindi Joseph.
Zao la alizeti limetajwa kuwa muhimu katika muktadha wa kupunguza changamoto ya mafuta nchini.
Hayo yamebainishwa jijini Dodoma na mbunge wa jimbo la Mchinga mkoani Lindi, Mama Salma Kikwete katika semina ya kujenga uelewa kwa wabunge wa mikoa ya Lindi na Mtwara.
Amesema Tanzania inaweza kujizalishia mafuta yake bila kutegemea mafuta kutoka nje ya nchi.
Kwa upande wao baadhi ya wabunge walioshiriki katika semina hiyo iliyoandaliwa na taasisi ya kuboresha Mifumo ya Masoko ya Kilimo Tanzania AMDT walikuwa na haya ya kusema.
Mkurugenzi Mtendaji wa taasisi ya kuendeleza mifumo ya masoko katika sekta ya kilimo Charles Ogutu amesema zao la alizeti ni muhimu katika kusaidia wakulima kujikwamu kiuchumi.