Wananchi Chali Isanga waahidiwa shule ya sekondari
22 June 2023, 4:14 pm
Wanafunzi wa kijiji hicho wamekuwa wakilazimika kutembea kilomita zaidi ya 16 kufuata shule ya sekondari Chokopelo.
Na Bernad Magawa.
Katibu mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Taifa Comredi Daniel Chongolo ameahidi kujenga shule ya Sekondari kijiji cha chali Isanga wilayani Bahi ili kuwaondolea adha wanafunzi waliokuwa wakitembea zaidi ya kilomita 16 kufuata sekondari kijiji cha Chikopelo.
Akizungumza kupitia ziara yake aliyoifanya wilayani Bahi Juni 21,2023 pia Chongolo ameahidi kujenga jengo la huduma za mama na mtoto pamoja na jengo la upasuaji ili kupunguza adha wanayoipata akina mama wa kata hiyo wakati wa kujifungua kwa kufuata kituo cha afya zaidi ya kilomita 20.
Mjumbe wa halmashauri kuu ya CCM Taifa Donard Mejiti naye akapata fursa ya kuzungumza na wananchi wa kata ya chali akaeleza kero ya kusuasua kwa Mradi wa maji kata ya chali.
Awali Mbunge wa Jimbo la Bahi Kenneth Nollo wakapata fursa ya kueleza changamoto zinazowakabili wananchi wa kata hiyo na kuomba utatuzi kutoka kwa katibu mkuu wa CCM.