Siku ya mtoto Afrika huadhimishwa kuangalia maslahi mapana ya watoto
16 June 2023, 1:28 pm
Siku ya mtoto wa Afrika inaadhimishwa kwa lengo la kuangalia maslahi mapana ya watoto wa Afrika na huwapasa watu wazima kujitolea kwa hali na mali ili kushughulikia changamoto zinazokabili watoto katika bara zima la Afrika pamoja na kulindwa dhidi ya ukatili na unyama wanaoweza kutendewa ndani na nje ya familia zao.
Na Alfred Bulahya
Mwaka 1991, wakuu wa nchi wanachama wa OAU walianzisha siku ya Mtoto wa Afrika kama kumbukumbu ya uasi dhidi ya wanafunzi 16 uliotokea Juni 1976 huko Soweto, Afrika Kusini.
Siku ya Mtoto wa Afrika ni siku inayosherehekewa kila mwaka tarehe 16 Juni katika kuenzi michango ya watoto walioshiriki katika maandamano kwenye mji wa Soweto, Afrika Kusini.
Siku hii maelfu ya watoto katika nchi ya Afrika Kusini walikusanyika katika mji wa Soweto kwa ajili ya maandamano yenye malengo ya kudai elimu bora, na kupinga aina ya elimu duni ya kibaguzi waliyopewa na serikali ya kibeberu.
Mamia ya watoto walipigwa risasi na kuuawa, huku watoto zaidi ya elfu moja wakijeruhiwa.
Nimezungumza na Bw. Eliaza Ngoda huyu ni mkurugenzi wa tasisi ya Recovery Youth with Vision (REYOVE) inayojihusisha na kuwasaidia vijana na watoto wanaoishi na kufanya kazi mtaani kuachana na matumizi ya dawa za kulevya.
Na nimeanza kwa kumuuliza hali ya uwepo wa watoto wanaoishi na kufanya kazi mtaani ikoje?