Ndaki ya sayansi UDOM yaanza programu huduma kwa jamii masomo ya sayansi
13 June 2023, 1:11 pm
Wana mpango wa kuweka ushirikiano na jiji la Dodoma idara ya elimu ili kufkia shule nyingi zaidi .
Na Mariam Matundu.
Ndaki ya sayansi asilia na hisabati kutoka chuo kikuu cha Dodoma (UDOM) wameanza programu ya huduma kwa jamii katika masomo ya sayansi na hisabati kwa kupitia shule nne zinazozunguka chuo kikuu cha Dodoma.
Rasi wa ndaki hiyo kutoka chuo kikuu cha Dododma Prof. Said Ally Vuai amezitaja shule hizo kuwa ni shule ya sekondari Iyumbu ,Ng’ongona, Sechelela na Ntyuka kwa lengo la kufundisha masomo ya sayansi hususani hisabati.
Aidha amesema kuwa wanampango wa kuweka ushirikiano na jiji la Dodoma idara ya elimu ili kufkia shule nyingi zaidi .
Mmoja wa wanafunzi wa kike anayesoma masomo ya sayansi katika sule ya sekondari Iyumbu ameomba jitihada hizo ziwafikie wanafunzi wengi ili kuongeza idadi ya wanafunzi wa kike kwenye masomo ya sayansi.