Kikundi cha vijana Mundemu kunufaika na kilimo cha nyanya
9 June 2023, 12:00 pm
Kikundi hicho kimepokea mkopo wa shilingi milioni nane kutoka halmashauri ya wilaya ya Bahi.
Na Bernad Magawa.
Kikundi cha kilimo tija cha vijana kijiji cha Mundemu kata ya Mundemu wilayani Bahi kinatarajia kunufaika na kilimo cha nyanya kupitia kilimo cha kitalu nyumba baada ya kikundi hicho kupokea mkopo wa shilingi milioni nane kutoka halmashauri ya wilaya ya Bahi.
Dinu Zeno ni mwenyekiti wa kikundi hicho chenye vijana watano wasichana wakiwa 2 na wavulana 3 ambao wamedhamiria kujikwamua kiuchumi kupitia kilimo anaelezea namna walivyojipanga kuhakikisha wanafikia malengo yao.
Naye diwani wa kata ya Mundemu Mheshimiwa Stanley Mtati amesema vijana hao watakuwa wa mfano kipitia mradi huo huku akiahidi kuwasaidia vijana kwa kuwasimamia vema ili fedha za serikali ziwe na tija kwa kwao.
Kwa upande wake Afisa tawala wa wilaya ya Bahi Jeremia Mapogo akizungumza mara baada ya kamati ya ulinzi na usalama ikiongozana na wakuu wa Idara wilaya ya Bahi kutembelea mradi huo ambao upo katika hatua za awali kuanza kutekelezwa amesema wilaya ya Bahi ipo katika maandalizi ya kuupokea mwenye wa uhuru mwezi Septemba 2023 hivyo Mradi huo wa kilimo wa vijana unaweza kuwa sehemu ya miradi itakayotembelea na Mwenge ili kuchocheea hamasa ya vijana kujiajiri.