Vijana walalamika kukosa mitaji ya kujiajiri
30 May 2023, 4:58 pm
Pamoja na serikali kutenga mikopo ya 10% kwa ajili ya vijana , akina mama na walemavu, bado kuna ugumu katika kupata mikopo hiyo.
Na Bernad Magawa
Katika kuhakikisha kuwa vijana hapa nchini wanajitengenezea ajira wenyewe badala ya kusubiri kuajiriwa, baadhi ya vijana wilayani Bahi mkoani Dodoma wameeleza kukosekana kwa mitaji kuwa ndicho kikwazo kikubwa cha wao kujiajiri.
Wakizungumza na kituo hiki vijana hao wameeleza ugumu wanaokutana nao wanapotaka kuanzisha biashara ndogondogo na kusema kuwa hakuna biashara unaweza ianzisha bila kuwa na fedha huku wakitoa ombi kwa serikali kuanzisha matamasha ya kutoa elimu ya ujasiriamali.
Wamesema pamoja na serikali kutenga mikopo ya 10% kwa ajili ya vijana , akina mama na walemavu, bado kuna ugumu katika kupata mikopo hiyo na kuiomba serikali kupunguza mashart ya upatikanaji ili vijana wengi wanufaike nayo.
Aidha wametoa wito kwa vijana wenzao kutokukata tamaa ya maisha na kuepuka makundi hatarishi yanayoweza kuharibu mwelekeo wa maisha yao.