Vijana watakiwa kujikita katika kilimo
25 May 2023, 7:41 pm
Katika eneo hili mazao mbalimbali yanazalishwa ikiwemo matunda kama vile embe papai na chungwa pamoja na mazao mengine kama migomba na mihogo.
Na Thadei Tesha.
Vijana jijini Dodoma wameshauriwa kujiingiza katika shughuli za kilimo kwani zikifanywa kiukamilifu zinaweza kuleta fursa na kusaidia kujikwamua kiuchumi.
Dodoma Tv imetembelea moja ya mradi wa kilimo uliopo katika makao ya watoto Kikombo na kushuhudia mradi wa kilimo cha matunda na mazao mengine ukifanyika katika eneo hilo.
Msimamizi wa shamba hilo ambaye pia ni afisa kilimo anaelezea juu ya mazao yanayozalishwa katika eneo hilo na mbinu wanazotumia kuzalisha mazao katika shamaba hilo.
Aidha anawashauri vijana kujiingiza katika fursa ya kilimo kutokana na umuhimu wake huku akisema kuwa kutokana na mkoa wa dodoma kuwa na udongo wenye rutuba kwa ajili ya kuzalisha mazao mbalimbali.