Mgogoro wa maji Subugo kutafutiwa ufumbuzi
19 May 2023, 3:45 pm
Viongozi wa Kijiji wametakiwa kuwa wabunifu kutambua fursa za kiuchumi zilizopo katika maeneo yao kama kilimo chenye tija ili waweze kuwakwamua wananchi kiuchumi na kupata maendeleo.
Na Bernadetha Mwakilabi.
Mgogoro wa maji uliopo kitongoji cha Subugo kati ya Serikali ya Kijiji Cha Pingalame, mzabuni wa kuchimba Kisima na mwalimu uliodumu Kwa muda wa zaidi ya miaka mitatu umetajwa kutafutiwa ufumbuzi wa kumaliza mgogoro huo ili wananchi waendelee kupata huduma ya maji.
Akiongea katika mkutano wa hadhara na wananchi wa Kijiji Cha Pingalame Mkuu wa wilaya Kongwa Mheshimiwa Remidius Mwema Emmanuel akiwa pamoja na kamati yake ya ulinzi na usalama amesema kutokana na utata uliopo ataunda timu maalumu ya wataalam kufatilia Kwa undani mgogoro huo kubaini ukweli na kuutatua.
Katika mkutano huo Mwema amepokea kero mbalimbali zikiwemo migogoro ya mipaka, ukosefu wa huduma za jamii kama umeme na afya ambapo ameahidi kuzimaliza na kuwasihi wananchi kuanza kuonesha nguvu kazi yao na Serikali kuwaunga mkono.
Akiongea kwa niaba ya wananchi Mwenyekiti wa Kijiji Cha Pingalame Bwana Sospeter Reuben amekiri kuwepo kwa changamoto hizo katika kitongoji cha Subugo.