Dodoma FM
Wananchi wahimizwa kuendelea kuchangia damu
15 May 2023, 8:10 pm
Uchangiaji wa Damu bado unatajwa kuwa muhimu katika kuokoa maisha ya watu wenye uhitaji.
Na Mindi Joseph.
Mwitikio wa Wanafunzi,Taasisi na wadau mbalimbali kuchangia Damu umetajwa kuondoa uhaba wa damu na kuvuka malengo ya uchangiaji katika kitengo cha Damu salama Mkoani Dodoma.
Taswira ya habari imezungumza na Renatus Mayunga Afisa Mteknolojia Hospital ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma na mhamasishaji wa uchangiaji damu ameyabainisha hayo leo katika zoezi la wadau waliojitolea kuchangia Damu.
Amesema wamefanikiwa kukusanya zaidi ya unit 350 za damu kwa kila mwezi na kuvuka malengo.
Kwa upande wake Mkuu wa Kanda ya Kati Vodacom Bw.Joseph Sayi anasema wamechagia damu kwa lengo la kuimarisha afya ya mama na mtoto.