Wakulima wa alizeti Bahi wahimizwa kuzingatia matumizi sahihi ya pembejeo
15 May 2023, 6:48 pm
Wakulima wa alizeti Bahi wahimizwa kuzingatia matumizi sahihi ya pembejeo ili kuzalisha zao hilo kwa wingi na ubora unaotakiwa nchini.
Na Bernad Magawa
Wakulima wa zao la alizeti wilayani Bahi wameshauriwa kutumia kwa usahihi pembejeo za kilimo ili waweze kuwa na mavuno mazuri katika zao hilo ambalo kwa sasa linahimizwa na serikali ikiwa ni mkakati wa kupunguza uhaba wa mafuta ya kupikia hapa nchini.
Abia Silungwe ni Afisa Ugani kata ya Lamaiti wilayani humo ameeleza kitaalamu umuhimu jambo hilo pamoja mbegu bora zinazofaa kwa kilimo hicho.
Aidha ametanabaisha namna wataalamu wa kilimo na Serikali inavyowasaidia wakulima kufikia malengo tarajiwa huku akitoa wito kwa wakulima kuipenda kazi hiyo kwani ni uti wa mgongo kwa taifa.
Awali baadhi ya wakulima wilayani humo waliishukuru serikali kwa kuwapatia pembejeo za kilimo kwa bei nafuu huku wakiomba serikali kuemndelea kutoa elimu zaidi kwa wakulima wa zao hilo.