NEEC na Bodi ya wakala wa uwezeshaji wananchi Zanzibar zasaini mkataba wa ushirikiano
12 May 2023, 1:18 pm
Tukio hilo la utiaji Saini limefanyika katika ofisi za baraza la Taifa la uwezeshaji wananchi kiuchumi zilizopo eneo la Nzuguni jijini Dodoma.
Na Fred Cheti.
Baraza la Taifa la uwezeshaji wananchi kiuchumi (NEEC) pamoja na Bodi ya wakala wa uwezeshaji wananchi kiuchumi Zanzibar zimesaini mkataba wa ushirikiano wa kazi zao za uwezeshaji wananchi kiuchumi.
Tukio hilo la utiaji Saini limefanyika katika ofisi za baraza la Taifa la uwezeshaji wananchi kiuchumi zilizopo eneo la Nzuguni jijini Dodoma ambapo Mtendaji mkuu wa baraza la NEEC Bi Beng’i Issa anaeleza lengo la makubaliano hayo.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa bodi ya wakala wa uwezeshaji wananchi kiuchumi kutoka Zanzibar Bwana Juma Mohamedi pamoja na Mkurugenzi wa wakala wa Uwezeshaji Bwana Juma Burhan Zanzibar nao wanaelezea jinsi ambavyo ushirikiano huo utakua na tija.