Dodoma FM

Wanafunzi wawili wafariki Dunia na wengine 31 kujeruhiwa katika ajali ya gari

12 May 2023, 12:19 pm

Mkuu wa wa mkoa wa Dodoma Mh. Rosemary Senyamule akiwa na Katibu Tawala wa Dodoma mh. Ally Gugu wakiwajulia hali majeruhi wa ajali hiyo .Picha na Mkoa wa Dodoma.

ASP Ramadhani amesema kuwa chanzo cha ajali hiyo ni mwendokasi kasi uliosababisha gari kumshinda dereva kuacha njia na kupinduka ambapo hadi sasa dereva huyo anashikiliwa na Jeshi la Polisi wilayani humo.

Na Bernad Magawa

Wanafunzi wawili wa shule ya sekondari Mpalanga wilayani Bahi wamefariki dunia na wengine 31 kujeruhiwa baada ya gari walilokuwa wakisafiria kuacha njia na Kupinduka katika kijiji cha Chidilo wilayani humo.

Akizungumza na wananchi wilayani Bahi Mkuu wa mkoa wa Dodoma Mheshimiwa Rosemary Senyamule ametoa pole kwa wazazi waliofiwa na watoto pamoja na wale ambao watoto wao wamejeruhiwa katika ajali hiyo na kusema kuwa Serikali itagharamia matibabu kwa majeruhi pamoja na mazishi kwa waliofariki.

Sauti ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma.

Naye Mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama wilaya ya Bahi ambaye ni mkuu wa wilaya hiyo Mhe. Godwin Gondwe akitoa maelezo kwa Mkuu wa mkoa wa Dodoma alipofika wilayani humo kuwafariji wananchi ameeleza hatua za awali zilizochukuliwa na Uongozi wa wilaya mara baada ya kutokea kwa ajali hiyo.

Sauti ya Godwin Gondwe Mkuu wa wilaya ya Bahi.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma akizungumza na baadhi ya wanafunzi walio kuwa katika ajali hiyo . Picha na Mkoa wa Dodoma.

Kwa Mujibu wa Mkuu wa usalama Barabarani wilaya ya Bahi ASP Bakari Ramadhani amesema ajali hiyo imetokea Mei 11 majira ya Saa 5: Asubuhi ikihusisha gari lenye namba za usajili T. 519 BSY aina ya Mitsubishi Canter mali ya Bw. Abdul Rashid mkazi wa Dar-es salaam iliyokuwa imebeba wanafunzi 51,walimu 2 na dereva 1 ambao walikuwa wakielekea shule ya sekondari Magaga kushiriki mashindano ya michezo ya UMISETA.

.