Wakazi wa Nagulo waiomba Serikali kuwapatia huduma ya umeme
10 May 2023, 7:24 pm
Hivi karibu Serikali kupitia wizara ya Nishati wanakusudia kuongeza mafungu katika Mfuko wa Nishati Vijijini ili kuongeza kasi ya kufikisha umeme katika vitongoji 36,336 .
Na Victor Chigwada.
Inaelezwa kuwa nishati ya umeme ni muhimu kwa maendeleo ya jamii ikiwamo kuongeza ufanisi wa huduma za elimu,afya na sekta nyingine hivyo ikikosekana inaweza kuchelewesha maendeleo hususani katika jamii masikini
Hayo yanathibitishwa na wananchi wa kijiji cha Nagulo Kata ya Mpwayungu wakati wakiiomba Serikali kuwasambazia nishati hiyo katika vitongoji vyao ili kuongeza chachu ya kukuza maendeleo
Mwenyekiti wa kijiji hicho Bw.Meshaki Matonya ametoa wito kwa Serikali kukamilisha usambazaji wa umeme katika vitongoji ili kusaidia kurahisisha msukumo wa maisha
Kwa upande wake Diwani wa Kata ya Mpwayungu Bw.Antony Sakalani amesema kuwa usambazaji wa nishati hiyo ndani ya kata yake ni hafifu kwani umeme uliopo haujawafikia wananchi wengi wa vitongoji vya pembezoni
Sakalani ameongeza kuwa bado wanaendelea na jithada za kuwaomba mamlaka husika ya nishati hiyo kuhakisha wanakamilisha usambazaji wa umeme kwa vitongoji vilivyo baki