NEMC yatoa mrejesho juu ya kufungia sehemu zenye kelele chafuzi
9 May 2023, 3:11 pm
Mnamo tarehe Moja Mei mwaka huu baraza hilo la Taifa la uhifadhi na usimamizi wa Mazingira (NEMC) lilitangaza kuanza opresheni ya kukamata na kufungia maeneo ya kumbi za strehe,nyumba za ibada pamoja na maeneo mengine yanayosababisha mitetemo na kelele kinyume na sheria .
Na Fred Cheti.
Baraza la Taifa la uhifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) jana limetoa taarifa yake juu ya mrejesho wa operesheni ya kukamata na kufungia maeneo ya starehe na ibada yanayodaiwa kusababisha kelele chafuzi.
Opresheni hiyo imefanyika kwa muda wa wiki moja kuanzia Mei Mosi mwaka huu hadi Mei 7 ambapo taarifa hiyo ya mrejesho wa kilichofanyika imetolewa na Mkurugenzi mkuu wa Mamlaka hiyo Dkt. Samuel Gwamaka wakati akizungumza na waandishi wa habari.
Aidha Dkt. Gwamaka amewataka wamiliki wa maeneo yote waliyoyafungia kufuata masharti haya endapo watahitaji kufunguliwa ili waendelea na shughuli zao.