Madiwani waomba umeme katika Vitongoji
1 May 2023, 2:49 pm
Mrindoko amesema kutakuwa na SWITCHING STATION eneo la mbande itakayosaidia upatikanaji wa umeme pale inapotokea tatizo eneo Moja lisilete ukosefu wa umeme eneo lingine.
Na Bernadetha Mwakilabi.
Waheshimiwa madiwani ambao ni wawakikishi wa wananchi wameomba huduma ya umeme kwenye vitongoji wanavyosimamia Kwani Kuna vitongoji havijapata huduma hiyo mpaka Sasa.
Wakipokea taarifa za taasisi mbalimbali madiwani wa wilaya ya Kongwa wametoa rai yao Kwa kaimu meneja TANESCO wilaya Kongwa kuwasaidia kufikisha umeme katika vitongoji na kuangalia namna ya kufanya Kwa maeneo yenye umeme mdogo ili kuwasaidia wananchi kupata huduma za kusaga karibu na maeneo yao.
Akijibu maswali hayo kaimu meneja wa TANESCO wilaya Kongwa bwana Musa Mrindoko amesema kuwa ofisi imepokea na kuahidi kufanyia kazi suala la upatikanaji wa umeme vitongojini Kwa awamu ya pili Kwani awamu ya kwànza ililenga kuvifikia vijiji ambapo walifànikiwa Kwa asilimia 100.
Aidha Mrindoko ametoa rai kwa waheshimiwa madiwani kuongea na wananchi juu ya kuto haribu miundombinu ya umeme Kwani wanaweza kusababisha madhara ya ajali vifo na kukosa huduma ya umeme.