Millioni 30 kujenga uzio shule ya kigwe viziwi Bahi
20 April 2023, 10:28 am
Kukamilika kwa uzio huo kutawahakikishia usalama watoto shuleni hapo ambao wamekuwa wakiibiwa vitu mbalimbali zikiwemo nguo pamoja na vifaa vingine vya shule.
Na Bernad Magawa.
Katika kuendelea kutoa kipaumbele cha elimu kwa watoto wenye mahitaji maalumu hapa nchini, serikali imepeleka shilingi miliono 30 kujenga uzio wa shule ya viziwi kigwe ili kuimarisha usalama wa watoto hao katika mabweni wanayoishi.
Shule hiyo ambayo ni kongwe katika kutoa elimu ya mahitaji maalumu hususa ni watoto wenye matatizo ya kusikia ambayo ilianzishwa miaka thelathini iliyopita imekuwa na changamoto nyingi zikiwemo za usalama wa wanafunzi na mali zao kutokana na kukosa uzio.
Akizungumza wakati wa ziara ya kamati ya Fedha uchumi na Uongozi ilipofika kukagua ujenzi huo Mwalimu Mkuu wa shule hiyo Thadei Mhwagila amesema fedha hizo zimetatua kwa kiasi kikubwa changamoto changamoto za wanafunzi na kueleza hali halisi ya ujenzi huo.
Katika hatua nyingine Mhwagila ameeleza kuwa kwa kiasi kikubwa fedha hizo zimekwisha tumika na kiasi kilichobaki kinatosheleza kumalizia kazi ndogondogo zilizosalia ambazo ni kupaka rangi msingi wa uzio huo na umaliziaji mwingine.
Mwenyekiti wa kamati ya Fedha uogozi na mipango ambaye ni pia ni Mwenyekiti wa halmashauri hiyo na mjuumbe wa mkutano mkuu wa CCM taifa Mhe. Donald Mejiti amesema kamati imeridhishwa na maendeleo ya ujenzi huo.