Dodoma FM
Wakulima Dodoma wasusia zao la muhogo
14 April 2023, 4:05 pm
Zao la muhogo ni muhimu kwa matumizi ya chakula na biashara kwani ni moja kati ya zao linalo stahimili ukame na hustawi katika maeneo yenye Mvua chache.
Na Mindi Joseph.
Zao la Muhogo Mkoani Dodoma limetajwa kususiwa na Wakulima kufuatia ukosefu wa teknolojia ambazo zina uwezo wa kuongeza thamani ya zao hilo.
Taswira ya habari imezungumza na wakulima katika Kijiji cha makag’wa ambapo wameeleza nini kimewasibu na kusababisha wao kuacha kulima zao hilo la muhogo.
Kwa upande wake Diwani wa kata ya makag’wa Solomon Samweli anaeleza jitihada anazofaya kuhamasisha wakulima kulima muhogo kijijini hapo.