Nishati mbadala kuwanufaisha wakazi wa Makang’wa
10 April 2023, 11:50 am
Mradi huo unaotekelezwa kwa fedha kutoka Mfuko wa umoja wa wanawake( UWT) wilayani humo unatarajia kunufaisha moja ya kikundi cha wanawake katika kijiji hicho.
Na Fred Cheti
Baadhi ya wanawake wa kijiji cha Makang’wa wilayani Chamwino wanatarajia kunufaika na mradi wa nishati mbadala ya kupikia inayotarajiwa kutengenezwa kupitia mabaki ya mazao.
Hayo yameelezwa na Diwani wa viti maalumu kutoka wilaya ya Chamwino Bi Dinna Menda wakati akifanya mahojiano na Dodoma Tv ambapo amesema mradi huo unaotekelezwa kwa fedha kutoka Mfuko wa umoja wa wanawake( UWT) wilayani humo unatarajia kunufaisha moja ya kikundi cha wanawake katika kijiji hicho.
Aidha Diwani huyo ameeeleza endapo mradi huo utakafanikiwa ni kwa kiasi gani utawasaidia wanawake katika eneo hilo kuondoka na matumizi ya nishati asilia ambayo si rafiki kwa mazingira.