Wananchi chemba wanufaika na elimu ya utunzaji ardhi
6 April 2023, 6:09 pm
Hali hii inatajwa kusababishwa na shughuli za kibinadamu ikiwemo kukata miti, uwepo wa milima iliyozungukwa na udongo wa kichanga usioweza kushinadana na kasi ya maji, hali inayotajwa na wataalamu kuwa na athari katika kilimo.
Na Mindi Joseph.
Baadhi ya wakulima wilaya ya Chemba Mkoani Dodoma wemesema wamenufaika na elimu ya Teknolojia za Kisasa za kukabiliana na Mmomonyoko wa udongo.
Wakizungumza na Taswira ya Habari wamesema teknolojia hiyo imewasaidia kufuatia kuwa katika hatihati ya kukosa mavuno ya kutosha katika msimu huu wa kilimo kutokana na mmomonyoko wa udongo.
Elirehema Swai ni Mratibu wa utafiti na Ubunifu Tari anasema udongo wenye rutuba shambani kwa wakulima umesombwa na kuacha mazao yakiwa na afya duni.