CCM yaagiza serikali kutekeleza miradi yote Wilayani Bahi
31 March 2023, 4:09 pm
Hii inafuatia kuhakikisha ilani ya chama hicho inatekelezwa kikamilifu na kuwaletea maendeleo wananchi.
Na Bernad Magawa.
Kamati ya siasa ya Chama cha Mapinduzi CCM wilaya ya Bahi imeiagiza Serikali wilayani humo kuhakikisha miradi yote inayotekelezwa wilayani humo inaendana sawa na thamani ya fedha iliyotolewa na serikali .
Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Bahi Stuwart Masima katika siku ya kwanza ya ziara ya kukagua miradi ya maendeleo iliyofanyika Machi 30,2023 ambapo jumla ya miradi 13 imetembelewa na kamati hiyo ikiwemo miradi ya Afya, elimu, pamoja na miundombinu ya barabara na stendi ya mabasi ya wilaya ya Bahi.
Akizungumza kuhusiana malalamiko ya wananchi kuhusu na adha inayohusu stendi ya Mabasi wilayani humo Mwenyekiti wa CCm wilaya ya Bahi amesema kamati haijaridishwa na thamani ya fedha iliyotumika katika kujenga stendi hiyo na kusema kuwa wananchi bado wanapata adha nyingi katika usafiri huku akiwaomba wananchi kuwa na subira wakati changamoto zao zikishughulikiwa.
Aidha Masima ameagiza majengo yote ya zahanati na vituo vya afya yanayojenwa wilayani Bahi kukamilika kwa wakati ili yaanze kutoa huduma kadiri ya maelekezo ya serikali.
Kaimu aimu mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Bahi Honolina Mukunda akipokea maelekezo ya kamati na kuahidi kuyafanyia kazi kwa wakat Insert.
Awali wakitoa taarifa katika miradi mbalimbali baadhi ya viongozi wameiomba kamati ya siasa kuwasaidia kutatua changamoto zinazowakabili zikiwemo changamoto mbalimbali zilizopo katika stendi ya mabasi ya wilaya ya Bahi.