Zaidi ya wananchi 2249 wapatiwa elimu ya kujikinga na MARBURG
30 March 2023, 6:52 pm
Wizara ya Afya kwa kushirikiana na wadau mbalimbali imefanikiwa kufikia makundi mbalimbali ya watu ikiwemo wahudumu wa afya ngazi jamii na Wahudumu wa Afya Vituoni.
Na Mindi Joseph.
Elimu ya kujikinga na ugonjwa wa Marburg imeendelea kutolewa kwa kila mtanzania tangu itolewe taarifa ya ugonjwa huo huku zaidi ya wananchi 2249 wamefikiwa na Elimu Nchini.
Taswira ya Habari imezungumza na Mtalaam wa Ufuatiliaji wa Magonjwa kutoka Wizara ya Afya, Emmanuel Mwakapasa ambapo amesema.
Katika hatua nyingine Mwakapasa ametaja dalili za Ugonjwa huo.
Kwa mujibu wa taarifa za Shirika la Afya Duniani (WHO), ugonjwa huo uligundulika kwa mara ya kwanza Ujerumani mwaka 1967 na ndio asili ya jina la ugonjwa huu na ulishawahi kutolewa taarifa katika nchi mbalimbali za Afrika na Ulaya .