Wakazi wa Ndogowe walazimika kutembea umbali mrefu kufuata huduma ya afya
24 March 2023, 4:19 pm
Kukosekana kwa baadhi ya huduma za afya katika zahanati ya kijiji cha Ndogowe imesababisha wananchi kutopata huduma ya afya hali inayowalazimu kutembea umbali mrefu kutafuta huduma hiyo.
Na Victor Chigwada.
Imeelezwa kuwa kukosekana kwa baadhi ya huduma za afya katika zahanati ya kijiji cha Ndogowe imesababisha wananchi kutopata huduma ya afya hali inayowalazimu kutembea umbali mrefu kufuata huduma hiyo.
Baadhi ya wananchi wa kijiji hicho wakizungumza na Taswira ya habari Wamesema kuwa uhaba wa majengo kwa ajili mapumziko na ,uhaba wa watumishi wa kike ni sababu nyingine inayosababisha hali ya huduma ya afya kusalia kuwa changamoto kubwa .
Katika kuendelea kufahamu hali ilivyo Taswira ya Habari imezungumza na Mwenyekiti wa kijiji cha Ndogowe Haruni Mlimuka ambaye amesema licha ya kufuata huduma ya afya mbali na kijiji hicho lakini changamoto ya barabara imekuwa sababu nyingine ya kukwamisha wananchi kufika huko zilipo huduma za afya.
Nae Diwani wa Kata ya Ng’hambaku Haruni Siengo amekiri kuwepo kwa changamoto ya watumishi katika zahanati hiyo hali inayodhoofisha upatikanaji wa huduma bora za afya.