Uongozi wa Shule za Ephiphany wamtaka mwekezaji kufuata sheria ili kuepusha mgogoro
20 March 2023, 4:17 pm
Mwekezaji huyo anaedaiwa kuingilia mpaka wa eneo la shule hiyo anadai kuuziwa eneo hilo na halamshauri husika.
Na Fredi Cheti.
Uongozi wa shule za Ephiphany zilizopo kata ya Mwegamile Wilayani Chamwino Mkoani Dodoma umejikuta ukiingia katika mgogoro wa kugombania mpaka na Mwekezaji anaedaiwa kuingilia mpaka wa eneo la shamba la shule hiyo.
Dodoma Tv ilifika katika eneo hilo na kushuhudia baadhi ya mazao katika eneo hilo yakiwa yameharibiwa ambapo Meneja wa shule hizo amedai jambo hilo limefanywa na mwekezaji huyo anaedaiwa kutaka kupitisha barabara katika eneo hilo bila kufuata utaratibu jambo linalotaka kuibua mgogoro baina yao.
Dodoma TV ilimtafuta Mwenyekiti wa kijiji cha Mwegamile ili kujua kama anafahamu kinachoendelea katika mgogoro huo na alikua na haya ya kusema.
Kwa mujibu wa taarifa zilizopo Mmiliki wa shule hizo anadaiwa kununua eneo hilo kwa wanananchi huku mwekezaji huyo anaedaiwa kuingilia mpaka wa eneo la shule hiyo akidaiwa kuuziwa na halamshauri ambapo Dodoma tv imezungumza na wananchi waliouza eneo hilo kwa mmiliki wa shule hizo za Epiphany na hapa wanaeleza jinsi ilivyokua.
Jitihada za kutaka kuzungumza na mwekezaji huyo anaedaiwa kuvamia eneo hilo ziligonga mwamba kutokana na kutokuwepo eneo la tukio hivyo suala hilo tutaendelea kufuatilia zaidi ili kujua hatma yake.