Jamii yatakiwa kuwa na muamko wa kuripoti matukio ya ukatili wa kijinsia
16 March 2023, 4:51 pm
Nini kifanye ili kutoa mwamko kwa jamii hasa kuanzia ngazi za familia na mitaa katika kuripoti matukio ya ukatili.
Na Fred Cheti
Jamii yatakiwa kuona umuhimu wa kushiriki katika kuripoti matukio ya ukatili wa kijinsia yanayotokea katika maeneo yao.
Hayo yameelezwa na baadhi ya wadau wa masuala ya kupinga ukatili wa kijisia wakati wakifanya mjadala katika kipindi cha SANUKA kinachorushwa kupitia dodoma redio ambapo wamesema ili kupunguza au kumaliza tatizo hilo ni lazima jamii ichukue hatua madhubuti katika kuyaripoti matukio hayo.
Nini kifanye ili kutoa mwamko kwa jamii hasa kuanzia ngazi za familia na mitaa katika kuripoti matukio ya ukatili? mwenyekiti wa Mtaa wa Nzinje Bwn Godfrey Samweli pamoja na mwenyekiti wa Mtaa wa Bwawani Michese Bwn Sospiter Maswepa wanashauri.
Halima Ibrahimu ni Mwanaharakati kutoka SMAUJATA anaelezea umuhimu wa jamii kuripoti matukio hayo huku akielezea athari zinazoweza kujitokeza endapo jamii itakaa kimya juu ya matukio hayo.