Uwepo wa wanyamapori kwaleta changamoto ya wanafunzi kuto udhuria masomo
14 March 2023, 4:44 pm
Uwepo wa wanyamapori na umbali wa shule ni changamoto inayosababisha wanafunzi wanaojiunga na masomo ya sekondari katika kata ya Ngh’ambaku Wilayani Chamwino kushindwa kuhudhuria masomo kwa wakati.
Na Victor Chigwada.
Umbali wa zaidi ya kilomita arobaini na usalama hafifu kutokana na uwepo wa wanyamapori ni changamoto inayosababisha wanafunzi wanaojiunga na masomo ya sekondari katika kata ya Ngh’ambaku wilayani Chamwino kushindwa kuhudhuria masomo kwa wakati.
Diwani wa Kata hiyo Bw.Haruni Siengo amekiri kukosekana kwa shule ya sekondari imesababisha wanafunzi kufuata huduma hiyo katika kata ya Mpwayungu yenye umbali wa zaidi ya kilomita orobaini
Siengo amesema kuwa licha ya umbali huo pia suala la eneo hilo kupakana na hifadhi ya ruaha imeongeza hatari kwa wanafunzi kutokana na uwepo wa wanayapori.
Naye Mwenyekiti wa Kijiji Cha Ndogowe Bw.Haruni Mlimuka amesema kuwa jitihada za kujenga sekondari tayari zipo kwenye mpango licha ya uwepo wa sintofahamu kuhusu nini kimekwamisha ujenzi huo.
Mlimuka amesema kukosekana kwa sekondari katika Kata yao kumesababisha baadhi ya wazazi kuwalazimisha watoto kufanya vibaya katika mitihani ya darasa la Saba ili kukwepa baadhi ya changamoto.
Aidha baadhi ya wananchi wa Kijiji Cha Ndogowe wametoa wito kwa jamii kuhakikisha wanaungana na wanashirikiana kwaajili ya ujenzi wa shule ya sekondari.
Kata ya Ngh’ambaku Ni moja ya maeneo yanayo pakana na hifadhi ya wanyamapori ya Ruaha hivyo Serikali kwa kushirikiana na mradi wa hifadhi ya jamii WMA waliamua kutenga eneo la hifadhi katika Kata hiyo kwaajili ya wanyama wanaoweza kuvuka mpaka wa Ruaha.