Wanawake watakiwa kusimama imara kupinga ukatili
8 March 2023, 4:04 pm
Wanawake wametakiwa kuwa mstari wa mbele katika kukemea na kupinga vitendo vya ukatili wa kijinsia vinavyo endelea katika jamii.
Na Mariam Kasawa.
Wanawake wametakiwa kuwa mstari wa mbele katika kukemea na kupinga vitendo vya ukatili wa kijinsia vinavyo endelea katika jamii.
Hayo yamesemwa na mwenyekiti wa umoja wa wanawake Tanzania {UWT } wilaya ya Dodoma mjini Bi. Zabibu Mtoro alipo kuwa akizungumza na wanawake wa kata ya Makulu walipokuwa katika zoezi la
upandaji miti ili kuadhimisha siku ya wanawake Duniani.
Amesema vitendo vya ukatili hususani kwa watoto wa kiume na wakike vimekithiri katika maeneo mengi hivyo viongozi na wananchi wanatakiwa kuungana kwa pamoja kukemea vitendo hivi.
Nae Mwenyekiti wa UWT kata ya Makulu bi Joha Ntonga amewataka wazazi kuendelea kuwalea watoto katika maadili pia wazazi wenyewe waepuke kuwafanyia watoto vitendo vya ukatili.
Akizungumza baada ya zoezi la upandaji miti lililofanyika katika shule ya msingi Msangalalee katibu kata wa CCM Dodoma Makulu Samson Mkopi alikuwa na haya yakusema.
Katika kuadhimisha siku ya wanawake Duniani ambapo kimkoa inafanyika leo wilayani Kondoa umoja wa wanawake Tanzania UWT kata ya Dodoma Makulu wameadhimisha siku hii kwa kupanda miti katika shule ya msingi Msangalalee huku zoezi hilo likiongonzwa na mwenyekiti wa UWT wilaya ya Dodoma Bi Zabibu Mtoro.