Wakazi wa Mahama waiomba Serikali huduma ya umeme
1 March 2023, 5:45 pm
Ikumbukwe Feb 15 Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan alishudia tukio kubwa la kihistoria la utiaji saini mikataba ya utekelezaji wa miradi ya umeme.
Na Victor Chigwada
Baadhi ya vitongoji vya kijiji cha Mahama vimeendelea kukosa huduma ya umeme hivyo wameiomba Serikali kupitia wizara ya Nishati na mamlaka husika kupitia wakakla wa usambazaji umeme vijiji REA kuwasaidia kupata huduma hiyo.
Mwenyekiti wa kijiji cha Mahama Bw.Asheri Mkosi amekiri kuwa na mapungufu ya nishati ya umeme kwani vitongoji vya Muungano, Hnonya na Mgongolofu hivyo kuwa na uhitaji mkubwa wa nishati hiyo
Aidha Diwani wa Kata ya Chilonwa Bw.Alpha Mtuza amesema kukosekana kwa nishati ya umeme katika vitongoji kumi imepelekea kutegemea matumizi ya nishati ya umeme wa jua katika shughuli zao za kila siku
Mtuza ameongeza kuwa kutokana na wingi wa vitogoji katika Halmashauri nzima wamebahitika kupata vitongoji viwili ambavyo ndivyo vitaanza kufikishiwa nishati ya umeme ukilinganisha na bajeti ya 2023/2024
Ikumbukwe Feb 15 Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan alishudia tukio kubwa la kihistoria la utiaji saini mikataba ya utekelezaji wa miradi ya umeme Tukio ambalo jumla ya mikataba 14 ilisainiwa baina ya wakala wa nishati vijini (REA) ikihusisha kupeleka umeme kwenye vitongoji 1,522 katika mikoa 9,
maeneo 336 ya wachimbaji wadogo wa madini na vituo vya afya ,pampu za maji 399 pamoja na kuwaunganisha wateja wa awali 108,178