TPHPA kudhibiti viuatilifu bandia
1 March 2023, 4:47 pm
Matumizi Sahihi na Salama ya Viuatilifu yanalenga kujali Afya ya Watu na Mazingira kwa maendeleo endelevu na Kulinda afya ya binadamu na mazingira kwa usimamizi endelevu na bora wa viuatilifu na afya ya mimea.
Na Fred Cheti.
Mamlaka ya Afya ya Mimea na viuatilifu TPHPA imeendelea kufanya ukaguzi wa mara kwa mara ili kudhibiti athari ya kuwepo kwa viuatilifu bandia.
Hii ni kufuatia Kuwepo na wauuzaji wa Viuatilifu na mazao ya mimea wasio waaminifu
Kaimu Mkurungezi Mkuu Mamlaka ya Afya ya Mimea na viuatilifu Dkt. Joseph C. Ndunguru ameyasema hayo leo jijini Dodoma wakati akizungumza na waandishi wa habari.
DKT Ndunguru Ameongeza kuwa bado Uelewa mdogo wa wakulima juu ya matumizi sahihi ya viuatilifu na hapa wakulima wanazungumza.