Uhaba wa vyumba vya madarasa watajwa kuwa kikwazo
22 February 2023, 5:38 pm
Uhaba wa vyumba vya madarasa na nyumba za walimu imetajwa kuwa kikwazo kikuu cha maendeleo.
Na Victor Chigwada.
Uhaba wa vyumba vya madarasa na nyumba za walimu imetajwa kuwa kikwazo kikuu cha maendeleo ya elimu katika kata ya Chilonwa Wilaya ya Chamwino.
Hayo yameeleza na mwenyekiti wa kijiji cha Mahama Bw.Asheri Mkosi ambapo amesema idadi kuwa ya wanafunzi haiendani na idadi ya vyumba vya madarasa vilivyopo pamoja na nyumba za walimu katika shule ya Msingi mahama.
Mkosi ameongeza kuwa wameanza jitihada za kuongeza vyumba vya madarasa ili kukabiliana na idadi ya wanafunzi pamoja na ofisi ya walimu.
Aidha ameiomba Serikali kuboresha suala la ujenzi wa nyumba za walimu ili kuwapunguzia gharama za kupanga pamoja na usafiri wa kila siku.
Naye Diwani wa Kata ya Chilonwa Bw.Alpha Mtuza amesema kuwa pamoja na changamoto hizo lakini wameendelea kupambana kuongeza vyumba vya madarasa kwa ushirikiano wa mbunge wa jimbo hilo.