Bilioni 1.172 kujenga barabara kongwa
16 February 2023, 3:46 pm
Wakala wa barabara za mijini na vijijini Tanzania (TARURA) wilayani kongwa wanatarajia kutumia shilingi Bilioni 1.172 kwaajili ya kujenga na kukarabati miundombinu ya barabara katika bajeti ya mwaka wa fedha 2023/2024.
Na Bernadetha Mwakilabi.
Meneja wa TARURA Kongwa injinia Peter Johnson amesema bajeti hiyo ambayo tayari imepitishwa na baraza la madiwani pia itajenga barabara ya kilomita moja katika eneo la Kongwa mji.
Aidha injinia Johnson ameeleza changamoto wanazokabiliana nazo katika ujenzi na uhifadhi wa miundombinu ya barabara na kutoa rai kwa wananchi katika utunzaji wa miundombinu hiyo.
Kukamilika kwa matengenezo na ujenzi wa barabara hizo utachochea kwa kiasi kikubwa kuondoa changamoto ya usafiri katika maeneo yaliyokuwa hayafikiki kutokana na ubovu wa barabara na kukuza uchumi kibiashara.