Dodoma FM

Vijana Chilonwa watakiwa kuchangamkia fursa ujenzi wa chuo cha Veta

10 February 2023, 2:18 pm

picha ya nembo ya VETA. Picha na Radio Tadio

Mwaka jana Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe Prof Adolf Mkenda alisema kuwa Serikali inayo azma ya kujenga Chuo cha Ufundi Stadi katika kila Mkoa na Wilaya nchini. Katika mwaka huu wa fedha 2022/2023, Serikali imetenga kiasi cha Shilingi Bilioni Mia moja (100 Bil).

Na Victor Chigwada                                                                

Vijana wa Kata ya Chilonwa Wilayani Chamwino wametakiwa kuchangamkia fursa ya ujenzi wa chuo cha ufundi (VETA) kinacho tarajiwa kujengwa ndani ya Kata hiyo.

Diwani wa Kata ya Chilonwa Bw.Alpha Mtuza amewasihi vijana ndani ya kata hiyo kuwa tayari kujishughulisha katika fursa hiyo  kwani ni moja  ya njia ya kujikwamua kiuchumi kupitia ujenzi wa chuo hicho.

Alpha Mtuza.

Naye mwenyekiti wa kijiji cha Mahama Bw.Asheri Mkosi amesema kuwa watahakikisha wanaendelea kutoa elimu na kuwahamasisha vijana kujiunga na mafunzo ya ufundi stadi

Asheri Mkosi

Aidha baadhi ya vijana wamesema kuwa kukosekana kwa mitaji na maeneo ya biashara imekuwa ikiwatia hofu kujiunga na mafunzo ya vyuo  na kuishia kubaki na mawazo yao kichwani

vijana