Dodoma FM

Shule ya Msingi Idifu yashindwa kuhimili wingi wa wanafunzi

6 February 2023, 5:33 pm

Baadhi ya majengo ya shule . Picha na facebook

Walipokea ahadi kupitia mfuko wa jamii TASAF lakini kutokana na kukosekana kwa utekelezaji imechangia kuwavunja moyo wananchi katika eneo hilo.

Na Victor Chigwana

Uchakavu na uchache wa madarasa katika shule ya Msingi Idifu  imetajwa kushindwa kuendana na Idadi ya wanafunzi waliopo hivi sasa

Hayo yamefahamika baada ya Taswira ya Habari kufanya Mahojiano na Mwenyekiti wa kijiji cha Idifu Bw.Atanasio Mgonhwa ambapo amesema kuwa pamoja na idadi kubwa ya watoto shuleni hapo lakini hali ya uchakavu wa madarasa bado ni tishio

Ameongeza kuwa licha ya kupata ahadi za wafadhili lakini utekelezaji wake umekosa nguvu ya Utatuzi.

Atanasio Mgonhwa.

Mgonhwa  amesema idadi hiyo ya wanafunzi imesababisha walimu kuzidiwa na wanafunzi  na kusababisha hali ya ufaulu katika shule hiyo kushuka zaidi

Mgonhwa

Naye Diwani wa Kata hiyo Bw.Samweli Kaweya amesema kuwa licha ya changamoto nyingi za kielimu lakini bado wameendelea na juhudi za uboreshaji wa elimu ndani ya Kata yao

Samwel Kaweya