Wilaya ya Bahi yapanga kuongeza kiwango cha ufaulu
2 February 2023, 4:07 pm
Wilaya ya Bahi yapanga kuongeza kiwango cha ufaulu kutoka nafasi ya kumi hadi ya tano kitaifa kwa mwaka 2023/2024.
Na Benard Magawa .
Halmashauri ya wilaya ya Bahi imeanza mikakati ya kuhakikisha wanapandisha zaidi ufaulu kwa mwaka 2023 lengo likiwa ni kushika nafasi ya tano kitaifa.
Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa kamati ya Elimu Afya na Maji wilayani humo ambaye pia ni Diwani wa kata ya mpamantwa Mheshimiwa Sostenes Mpandu alipokuwa akiwasilisha taarifa ya kamati hiyo katika kikao cha Baraza la Madiwani kilichofanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Halmashauri ya Bahi.
Mheshimiwa Mpandu alisema moja ya mikakati waliyonayo ni pamoja na kutoa motisha kwa walimu wanaofanya vizuri wakiwemo Afisa Elimu wa shule za msingi na Sekondari wilayani humo ambao wanatarajia kuwapa vyeti vya pongezi namoja na shilingi 100,000/= kila mmoja kwa mchango wao mkubwa uliyoipatia sifa kubwa wilaya hiyo.
“Alisema wilaya ya Bahi imekuwa halmashauri ya wilaya pekee iliyoingia katika nafasi za kumi bora kitaifa huku ikiwa katika mchuano mkali.”
Baadhi ya madiwani waliohudhuria kikao hicho akiwemo Diwani wa kata ya kigwe Mheshimiwa Adoln Mabalwe alisema mkakati mwingine wa kufikia malengo hayo ni kuwahudumia walimu kwa haraka wanapofika halmashauri kutafuta huduma ili wawahi kurudi kuendelea na kazi za kufundisha.
“Akizungumza katika kikao hicho Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Bahi Athumani Masasi “
amelishukuru Baraza la Madiwani wilayani humo kwa usimamizi mzuri wa shughuli za halmashauri ambao umepelekea maendeleo s makubwa katika wilaya ya Bahi.