Mvumi Misheni walia na gharama za matibabu
23 January 2023, 11:47 am
Na; Victor Chigwada.
Licha ya huduma zinazotolewa katika hospitali ya Mvumi Misheni bado wananchi wametaja gharama za matibabu katika hospitali hiyo kuwa changamoto.
Hayo yameelezwa na mwenyekiti wa kijiji cha Mvumi Bw.Alpha Zoya wakati akizungumza na Taswira ya Habari ambapo amekiri kijiji chake kukosa huduma ya zahanati pamoja na kituo cha afya
Zoya amesema ili kupata huduma hiyo wananchi hulazika kupata huduma katika hospitali ya DCT ambayo inagharama kubwa licha ya ahadi ya ujenzi wa kituo cha afya
Aidha ameongeza kuwa wameendelea kutoa elimu kwa wananchi juu ya ukataji wa bima ili kuondokana na malalamiko ya gharama za matibabu
Naye Diwani wa Kata hiyo Bw.Keneth Chihute amekiri wananchi wa Kata yake kukosa huduma za afya kikamilifu kutokana na ukosefu wa kituo cha afya
Chuhute amesema kuwa kwasasa wananchi wanategemea huduma ya afya katika hospitali ya DCT
Hospitali ya Mvumi ni hospitali pekee Dodoma vijijini yenye uwezo wa kuhudumia zaidi ya watu laki nne kwa mwaka