Dodoma FM

Kata ya majeleko yakamilisha ujenzi wa madarasa

2 December 2022, 6:52 am

Na ;Victor Chigwada .    

Ujenzi wa vyumba vya madarasa unaendelea kuwa kipaumbele katika maeneo mengi nchini ili kuendana na sera ya elimu bila malipo ambayo imechangia kuongeza idadi ya udahili wa wanafunzi.

Mwenyekiti wa kijiji cha Chinangali one Kata ya Majeleko Bw.Stephano Kamoga ameeleza kuwa tayari wamekamilisha ujenzi wa vyumba vya madarasa wakishirikiana na viongozi mbalimbali wa Serikali

Kamoga ameongeza kuwa changamoto kubwa imekuwa ni kukosekana kwa daraja kwani uwepo wa korongo imekuwa changamoto kubwa kwa wanafunzi kipindi cha mvua

.

Diwani wa Kata ya Majeleko Bw.Mussa Omary amekiri kukamilisha ujenzi wa vyumba vya madarasa kwa asilimia kubwa ndani ya Kata yake vitakavyo saidia kuondokana na mlundikano wa wanafunzi

.

Pamoja na mafanikio hayo ya ujenzi wa vyumba vya madarasa lakini baadhi ya wazazi na wanafunzi wamelalamikia kukosekana kwa daraja imekuwa ikiwawia vigumu kufika shuleni hususani msimu wa mvua

.

Mussa Omary diwani wa Kata hiyo amesema kuwa kwasasa tayari wana mpango wa kushughulikia ujenzi wa daraja hilo kutokana na mradi wa upanuzi wa barabara

.

Uwepo wa changamoto ya  makorongo makubwa kwa baadhi ya maeneo imekuwa ikihatarisha usalama wa watoto hususani wanapo hitaji kuvuka kwenda upande wa pili kufuata huduma ya elimu