Wananchi watakiwa kujitokeza kupata elimu ya utalii.
23 November 2022, 1:45 pm
Na; Benard Filbert.
Wakazi wa Mkoa wa Dodoma wameombwa kujitokeza kwenye tamasha la utalii katika eneo la Nyerere square tarehe 26 mwezi huu kwa lengo la kupata elimu ya utalii.
Hayo yameelezwa na Dorothea Masawe kutoka Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA)kanda ya kati wakati akizungumza na Dodoma Fm kuhusu tamasha hilo.
Amesema wakazi wa Dodoma wanayo nafasi kubwa yakupata elimu ambayo itawasaidia kutembelea hifadhi ya mapori ya akiba yaliyopo mkoani Dodoma.
.
Hata hivyo ameema tamasha hilo limelenga kuelimisha wakazi wa Dodoma kuhusu suala la utalii huku wakiambatana na kampuni mbalimbali za utalii nchini.
.
Naye Emanuel Makwisa afisa uhifadhi wa TAWA kanda ya kati amesema ni fursa kwa wakazi wa Dodoma kuja katika tamasha hilo ili kuonja ladha ya nyama ya wanyapori ili kujivunia hifadhi zilizopo Dodoma.
.
Dodoma ni moja ya mkoa ambao una mapori ya akiba ambayo yanawanyama ambayo ni Pori la Mkungunero pamoja na Swagaswaga ambayo yanapatikana katika wilaya ya Chemba.