Zaidi ya billioni 474 zinatumika kuagiza mafuta nje ya Nchi
16 November 2022, 12:28 pm
Na; Mariam Matundu.
Imeelezwa kuwa iwapo mkakati wa kukuza na kuongeza uzalishaji katika zao la alizeti ukifanikiwa,serikali itafanikiwa kuokoa fedha nyingi ambazo zinatumika kuagiza mafuta ya kula nje ya Nchi .
Akizungumza katika mahojiano maalumu na Dodoma fm naibu waziri wa kilimo Mh Anthony Mavunde amesema kwa sasa zaidi ya bilioni 474 zinatumika katika kuagiza mafuta nje ya Nchi.
Naibu waziri wa kilimo amesema kuwa serikali imewekeza katika kuimarisha taasisi ya utafiti wa kilimo na wakala wa mbegu ambapo bajeti yake imeongezeka maradufu.
.
Aidha amesema katika kuhakikiza mkakati wa kukuza kizimo kwa 10% ifikapo 2030 serikali imepanga kuwa na mashamba makubwa ya pamoja elf kumi ifikapo 2030 ambapo kwa kuanza imeanzia mkoa wa Dodoma na Mbeya.
.
pamoja na hayo amesema upo mpango wa kugawa mbegu za ruzuku za alizeti ambapo itakuwa msaada mkubwa kwa wakulima.
.
Kwa sasa uzalishaji wa mafuta nchi ni tani laki mbili na elfu tisini ambapo mahitaji tani laki 6 na elfu hamsini kwa mwaka