Wilaya ya Kongwa yatarajia kuanza ujenzi wa vyumba 70 vya madarasa
5 October 2022, 2:23 pm
Na; Alfred Bulahya.
Halmashauri ya wilaya ya Kongwa Mkoani Dodoma, imepokea kiasi cha fedha shilingi bilion moja na milioni mia nne kwa lengo la ujenzi wa vyumba vipya 70 vya madarasa kwa ajili ya wanafunzi watakaofaulu mtihani wa darasa la saba.
hayo yamebainisha leo na Mkurugenzi mtendaji wa wilaya hiyo Dkt Omary Nkullo, wakati akizungumza na Taswira ya habari ofisini kwake.
Amesema pesa hizo zitatumika katika ujenzi wa madarasa 70 katika shule 23 za sekondari wilayani humo ili kuandaa mazingira bora na rafiki kwa wanafunzi watakaofaulu mitihani ya kuhitimu elimu ya msingi iliyoanza mapema hii leo.
.
Katika hatua nyingine amekemea tabia ya wazazi na walezi wilayani humo kuwaambia watoto wafanye vibaya katika mitahani yao ili wasifaulu kwa lengo la kukwepa gharama.
.
Nao baadhi ya watahiniwa kutoka shule ya msingi mnyakongo wameeza namna walivyojiandaa na mitihani hiyo wakisema wako tayari kufanya vyema kulingana na maandalizi waliyopata kutoka kwa walimu wao.
.
Jumla ya watahiniwa 10, 654 wanatarajia kufanya mitihani hiyo wilayano humo kwa muda wa siku mbili ambazo ni leo oct 5 na kesho octoba 6 mwaka huu.