Wanafunzi wanao hitimu darasa la saba watakiwa kuto jiingiza kwenye uhalifu
4 October 2022, 12:03 pm
Na; Victor Chigwada
Wito umetolewa kwa wanafunzi wanao hitimu elimu ya msingi kuacha kujihusisha na vikundi vya uhalifu ambavyo vimekuwa gumzo kwa hivi karibuni wakati wakisubiri matokeo ya mtihani.
Wito huo umetolewa na fadhila Chibago Diwani wa Kata ya Dodoma Makulu wakati wa mahafali ya darasa la saba katika shule ya Msingi Ihumwa ambapo amewapongeza watahiniwa hao huku akiwasihi kutojihusisha na makundi ya uhalifu wawapo mtaani
.
Aidha amesema ni vyema wanafunzi na wazazi kutumia fursa ya elimu katika kujikwamua kimaisha .
.
Akizungumzia mpango wa kata katika kukabiliana na Idadi kubwa ya wanafunzi Chibago amesema watahakikisha wanasimamia na kushirikiana na Halmashauri ili kuweza kukamilisha ujenzi wa shule mpya itakayo punguza msongamano wa wanafunzi hao
.
Kwa upande wake Diwani wa Kata ya Ihumwa Bw.Edwadi Mgawa amesema Kwasasa Wana mpango mkakati wa kuhakikisha wanakamilisha ujenzi wa shule mpya walio uanziasha
Hata hivyo katika kuhakikisha shule inapiga hatua katika ufaulu wamefanikiwa kupata ufadhili kupitia kanisa katoliki ambao umewezesha shule hiyo kufundishia kupitia vishikwambi .
.
Shule ya Msingi Ihumwa ni Miongoni mwa Shule Kongwe Mkoani Dodoma ambapo mahafali hayo ni ya 61 huku bado ikiendelea kukabiliwa na upungufu wa vyumba vya madarasa .