Dodoma FM

Kamati ya bunge yaridhishwa na mradi wa Timiza malengo

5 September 2022, 1:30 pm

Na; Benard Filbert.

Kamati ya Kudumu ya Bunge inayosimamia Masuala ya  UKIMWI, Kifua Kikuu , Dawa za Kulevya na Magonjwa yasiyoambukiza imeridhishwa na utekelezaji wa mradi wa Timiza Malengo unaotekelezwa na Tume ya Kudhibiti UKIMWI Tanzania (TACAIDS) unaolenga kuwawezesha vijana kiuchumi.

Hayo yamesemwa na Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Dkt. Alice Kaijage wakati wa ziara ya Kamati ilipotembelea na kukagua utekelezaji wa  mradi huo katika Halmashauri ya Mji wa Ifakara mkoani Morogoro

Amesema kuanzishwa kwa mradi kumewafanya vijana kuamka kifikra na kuamini  wana uwezo wa kujieletea maendeleo.

.

Naye  Naibu Katibu Mkuu , Ofisi ya Waziri Mkuu , Sera, Bunge  na Uratibu Bwa. Kaspar Mmuya  amesema  afua za UKIMWI hazitekelezwi na wizara moja pekee bali zinatekelezwa na  wizara zote za kisekta na wadau  wa ndani na nje ya Nchi .

.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Tume ya Kudhibiti UKIMWI Tanzania (TACAIDS), Dkt. Leonard Maboko  amefafanua tume hiyo inashirikiana  na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia ambapo ina mtaala wa uelimishaji rika ambao unafundishwa kwa wanafunzi wa shule za msingi na sekondari katika Halmashauri 18.

.

Mkuu wa Wilaya ya Kilombero mkoani Morogoro Bi. Hanji Godigodi ameipongeza Serikali kwa kuendelea kuunga mkono juhudi za taasisi za serikali na binafsi zinazopambana kudhibiti maambukizi ya virusi vya UKIMWI.

.

Mradi huo unatekelezwa ikiwa ni Awamu ya Pili kuanzia mwaka  2021 hadi  mwaka 2023 katika Halmashauri  za Wilaya 18 zilizopo katika  Mikoa mitano  ya Dodoma, Geita, Morogoro, Singida na Tanga ukihusisha vijana wanaotoka katika kaya masikini.