Dodoma FM

Magonjwa yasiyopewa kipaumbele yapelekea fuko wa bima ya Afya NHIF kuelemewa

1 September 2022, 2:04 pm

Na;Mindi Joseph .

Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu amesema uwepo wa ongezeko kubwa la magonjwa yasiyo ya kuambukiza imechangia kuelemewa kwa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF).

Kauli hiyo imekuja baada ya Kutokea kwa  sitofahamu iliyoibuka hivi karibuni kuhusu Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) kuelemewa na madeni ya matibabu ya wanachama wake huku  Waziri Ummy akiyataja magonjwa sugu kuwa chanzo.

Akizungumza leo Jijini Dodoma Waziri Ummy ametolea ufafanuzi kuhusu huduma na madai ya kuyumba kwa mfuko huo ambapo amesema uwepo wa ongezeko kubwa la magonjwa yasiyo ya kuambukiza inahatarisha uhai na uendelevu wa Mfuko huo.

Katika hatua nyingine amewataja watumishi wa NHIF kujiingiza katika tabia za udanganyifu wakishirikiana na vituo vya kutolea huduma za afya.

.

Kulingana na takwimu zilizopo, gharama za magonjwa yasiyo ya kuambukizwa zimeongezeka kutoka shilingi bilioni 35.65 mwaka 2016/17 hadi shilingi bilioni 99.09 mwaka 2021/22.

 

.

 

Kwa Mujibu wa takwimu hizi, ni wazi kuwa kama Nchi haitachukua hatua madhubuti kuna uwezekano wa Mfuko huo wa NHIF kwa siku za mbeleni kushindwa kutimiza majukumu yake kwa mujibu wa Sheria.