Athari za vilevi kwa wanawake wajawazi
20 July 2022, 2:00 pm
Na; Benard Filbert.
Matumizi ya vilevi kwa wanawake wajawazito imetajwa kuwa na athari kubwa ikiwepo kujifungua mtoto mwenye mgongo wazi.
Hayo yanajiri kutokana na baadhi ya watoto wanaokutwa na tatizo la mgongo wazi kutajwa kusababishwa na mama zao kutumia vilezi wakati wakiwa wajawazito.
Baadhi ya wakazi wameiambia taswira ya habari kuwa ni vyema wataalamu wa afya wakaendelea kuelimisha jamii kwa ujumla athari za kutumia vilevi hususani kwa wanawake wajawazito.
.
Peter Mabula ni daktari bingwa wa upasuaji tatizo la mgongo wazi kutoka hospital ya rufaa Dodoma amesema kuna uhusiano mkubwa kati ya mama mjamzito kutumia vilevi na kuzaliwa kwa mtoto mwenye mgongo wazi.
.
Wanawake wajawazito wanaaswa kaucha kutumia vilevi kipindi cha ujauzito ili kuepusha athari mbalimbali zinazoweza kujitokeza.