Hospitali ya Mirembe yafanya utafiti ili kuandaa elimu ya Saikolojia
20 June 2022, 2:34 pm
Na; FRED CHETI.
Katika kuendelea kuboresha utaoji huduma kwa wagonjwa wa akili hospitali ya Taifa ya Magonjwa ya afya ya akili Nchini Mirembe iliyopo jijini Dodoma imesema inafanya utafiti ili kuandaa muongozo mzuri wa elimu ya saikolojia kwa wagonjwa hao utakaotumika Nchini
Kauli hiyo imetolewa na Dkt. Paul Lawala Mkurugenzi Mkuu wa hospitali hiyo wakati akifanya mahojiano na wanahabari mara baada kumalizika kwa mkutano na wadau mbalimbli wa afya ya akili uliokua na lengo la kuwashirikisha juu ya tafiti hizo.
.
Dkt. Prasceda Swai ni Daktari bingwa wa Magonjwa ya akili kutoka hospitali ya Taifa ya Muhimbili nae ni miongoni mwa wanaondaa utafiti huo hapa anafafanua zaidi lengo lao
.
Ugonjwa wa akili ni moja kati ya Magonjwa ambayo huwapata watu wengi kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo msongo wa mawazo, ugonjwa na matumizi ya vilevi dawa za kulevya na sababu za kiimani.